Phillips atakiwa kusaidiwa
Kiungo wa kati wa Uingereza Kalvin Phillips anahitaji "msaada na watu wa kumsaidia", anasema meneja wa West Ham David Moyes.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 28 anadaiwa alinaswa akitoa ishara ya kuudhi kwa mashabiki wakati akipanda basi la timu baada ya kupoteza Jumamosi dhidi ya Newcastle United.
Phillips yuko kwa mkopo West Ham kutoka Manchester City hadi mwisho wa msimu huu. "Tunahitaji mashabiki wetu kuwapa wachezaji wetu wote sapoti wanayohitaji," alisema Moyes.
"Kalvin ni binadamu na anachohitaji ni msaada na watu wa kumsaidia, ndio tutafanya." Phillips amecheza mechi saba kwenye Premier League kwa upande wa London mashariki, akianza mara tatu pekee.
Aliingia akitokea benchi huko Newcastle na Wagonga nyundo wakiwa mbele kwa mabao 3-1 na kuona penalti ikitolewa dhidi yake ndani ya dakika 10 za kuwa uwanjani, kabla ya vijana wa Eddie Howe kunyakua 4-3.
"Kalvin ni mchezaji mzuri sana na ninaamini bado tunaweza kufanya kitu nje ya muda ambao tumekuwa naye hapa," alisema Moyes.
Phillips alijiunga na West Ham akilenga kurejesha nafasi katika kikosi cha England, hata hivyo Gareth Southgate alimwacha nje ya michezo ya hivi majuzi ya kirafiki ya kimataifa dhidi ya Brazil na Ubelgiji.
Southgate alisema: "Kwa sasa, sikuweza kuwa na uhakika juu ya uchezaji wa Kalvin katika wiki chache zilizopita kwamba anaweza kuingia uwanjani na kufanya kazi tunayojua kuwa anaiweza.